Michezo

Sasa ni rasmi huyu hapa Aubameyang ndani ya Arsenal (+picha)

Klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu England imekamilisha usajili  uliyoweka rekodi ya paundi milioni 56 kwa Pierre-Emerick Aubameyang anayetokea Borussia Dortmund.

Kupitia mtandao wao wa Twitter hii leo klabu ya  Dortmund imethibitisha kumalizana na Arsenal ambaye kwa sasa ndani ya the Gunners anakuwa mchezaji anayelipwa zaidi na kuweka rekodi ya timu hiyo kwa kupokea paundi 180,000 kwa wiki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anajiunga na Arsenal wakati wadau wa soka wakishuhudia Olivier Giroud akiekea Chelsea na Michy Batshuayi akihamia Dortmund kuziba pengo la Aubameyang.

Picha za Aubameyang akiwa katika jezi za Arsenal

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents