Habari

SAUDI ARABIA: Mfanyakazi wa ndani afungwa kwenye mti juani kwa siku 4, Mitandao ya kijamii yamuokoa ‘ningekufa sirudi tena’

Mfanyakazi wa ndani mjini Ryadhi nchini Saudi Arabia amenusurika kifo baada ya kufungwa kwenye mti uliokuwa juani na bosi wake kwa kosa la kuacha samani za ndani juani.

Mwanadada huyo aitwaye Acosta Baruelo, 26 ambaye ni raia wa Ufilipino amesema alifungwa kwenye mti baada ya kuacha baadhi ya samani za thamani juani.

Akielezea jinsi alivyonusurika kwenye adhabu hiyo ya kinyama, amedai kuwa alimuomba mfanyakazi mwenzie wa kike ampige picha kisha asambaze kwenye mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya mkononi.

Baada ya tukio hilo, picha hiyo ilianza kusambaa hadi kufikia Mei 9, 2019 tayari Jeshi la Polisi mjini Ryadh lilikuwa limeshaipata nyumba hiyo na kumuokoa mfanyakazi huyo.

Mama huyo aliyetekeleza adhabu hiyo, tayari ameshafunguliwa kesi ingawaje mtuhumiwa wake amesharudishwa nyumbani.

Kufuatia tukio hilo, Ubalozi wa Ufilipino nchini Saudi Arabia ulilazimika kumsafirisha mwanamke huyo kumrudisha nyumbani siku hiyo hiyo aliyookolewa na polisi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mfanyakazi huyo ni mama wa watoto wawili na alifika Saudi Arabia miezi 7 kwa kupelekwa na madalali wa wafanayakazi wa ndani.

Akielezea tukio hilo Mwanadada huyo amesema “Nawashukuru watu wote walionisaidia kurudi nyumbani na rafiki yangu aliyenisaidia wakati nimefungwa nilijua nitakufa sitarudi tena. Naishauri serikali ichunguze kuna wafanyakazi wengi kutoka Ufilipino wanahangaika nchini Saudia, wanakatwa mishahara wengine wanapunguziwa na hata kufichiwa passport zao,“.

Ripoti zinaeleza kuwa kuna zaidi ya watu milioni 2.3 kutoka Ufilipino wanaofanya kazi za ndani Mashariki ya kati.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents