Burudani

Sauti Sol wajitengenezea rekodi mpya Instagram

By  | 

Hakuna ubishi kuwa Sauti Sol ni kundi linalofanya muziki mzuri Afrika. Ubora wa nyimbo zao ndio umewafanya kiasi ambacho wiki hii wamefikisha followers milioni 1 kwenye mtandao wa Instagram.

Baada ya kufanikiwa kuongeza idadi hiyo, wasanii hao kupitia mtandao wa Twitter wamesherekea kwa kuandika, “#Goodmorning Apparently we’re the first Kenyan musicians to reach a million legit followers on @instagram . Damn it’s hard outchea. ????.”

Kwa hatua hiyo kuna uwezekano mkubwa mpaka sasa kundi hilo ndio likawa la kwanza kuwa na idadi kubwa ya followers katika mtandao huo.

Wasanii hao kwa sasa wapo kwenye ziara ya show zao nchini Ujerumani na Ubelgiji.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments