Habari

Sauti za Busara lamalizika na kuitosa Bongo Flava kwa mara nyingine

2

Tamasha la kubwa la muziki Afrika Mashariki la Sauti za Busara limemalizika jana visiwani Zanzibar baada ya kuanza February 14. Sauti za Busara ni tamasha kubwa na linafahamika kama ‘Tamasha rafiki zaidi duniani’ huku mamia kwa maelfu wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine nchini hujumuika na raia wa kigeni kushuhudia wasanii wakitumbuiza.

Hata hivyo pamoja na kufanyika katika ardhi ya Tanzania ambapo muziki wa Bongo Flava umetawala mawimbi ya radio, wasanii hao hawana umaarufu wowote katika Sauti za Busara. Kwa muda mrefu tamasha hilo limekuwa likitilia zaidi mkazo kwa wanamuziki wanaofanya muziki wa kiafrika zaidi na unaopigwa live.

Mwaka huu msanii pekee anayefanya muziki huo aliyefanikiwa kupanda kwenye stage ya tamasha hilo ambalo hufanyika Ngome Kongwe, Zanzibar ni Peter Msechu.

7

Mwenyekiti wa Busara Promotions Simai Said aliliambia gazeti la Daily News kuwa hata wananchi wa Zanzibar na wengine kutoka Tanzania bara wanaoenda kushuhudia tamasha hilo hutaka kuwaona wanamuziki wakipiga vyombo vya muziki live.
4

Aliongeza kuwa hata mapromota wanaohudhuria tamasha hilo hutaka kuwaona wasanii wanaoweza kutumbuiza nyimbo zao live. “It’s a difficult thing for us to say I’m sorry but we cannot take you on stage,” aliliambia Daily News.

“In a way, if we do so we’re actually discouraging local artistes and ruining the talent they have, instead of taking them to different and higher levels. So we want to help the local musicians but what we are saying is that you have to try harder and find a way to create your own unique style to come up,” aliongeza.

3

Lakini pamoja na ukweli huo kuwa wasanii wengi wa Bongo Flava hawapigi live, Sauti za Busara ambayo huwa ni jukwaa zuri kwa wasanii wa ndani kujitangaza kwa wapenzi wa muziki kutoka nje ya nchi liendelee kutawaliwa na muziki kutoka mataifa mengine?

5

“Haiwezekani ikawa wasanii wa kigeni kila mwaka wanakuja na kutawala tamasha hilo, eti kwa sababu wasanii wetu hawajui kutumia vyombo vya muziki katika kutumbuiza jukwaani,” umeandika uchambuzi kwenye gazeti la Mwananchi la leo Feb 18.

Damian Mihayo akiimba pamoja na Peter Msechu
Damian Mihayo akiimba pamoja na Peter Msechu
Mtoto akitazama performance kwenye tamasha hilo
Mtoto akitazama performance kwenye tamasha hilo

“Sisi tunaamini, ipo haja kubwa ya wasanii wetu kuwezeshwa vifaa vya muziki ili waweze kujifunza na kuvitumia vifaa hivyo badala ya kuwaacha wasanii hawa wa Bongo Fleva wakiaibika. Tunaamini kwamba wasanii wa Bongo Fleva wanashindwa kutumia vyombo vya muziki, wanakosa ubora wa sauti na wana udhaifu wa ujumbe katika tungo zao kwa sababu hawawezeshwi hata kidogo, na kwamba wanayoyafanya mpaka wanafahamika ni juhudi zao binafsi tu.

10

11

Untitled

“Sisi tunaamini vijana hawa wa Muziki wa Bongo Fleva wakiwezeshwa vifaa vya muziki na wakipewa mafunzo ya muziki watabadilika na muziki wa Bongo Fleva utapendwa zaidi ndani na nje ya nchi. Tunasema hivyo kwa sababu tunafahamu ni wasanii wachache wa muziki wa Bongo Fleva wenye uwezo wa kununua gitaa angalau moja kwani vifaa vya muziki vinauzwa bei kubwa na wanamuziki wengi vipato vyao vya chini,” ulisisitiza uchambuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents