Habari

Sauti za Busara yaanza kupokea filamu za muziki


Tamasha la Sauti za Busara limekubali kupokea filamu za muziki kwaajili ya mpango wake wa African Music Film wa mwaka 2013.
Msimu wa kumi wa tamasha hilo umepangwa kufanyika kuanzi tarehe 14- 17 February, 2013 kwenye eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar.
Tamasha la Sauti za Busara linatafuta filamu zenye urefu wa aina mbalimbali, zinazovutia na kuburudisha kutoka kila eneo la Africa.
Zinaweza kuwa clip za muziki, tamasha lililorekodiwa, documentary za muziki n.k. Filamu bora zitachaguliwa na kuoneshwa kwenye tamasha hilo.
Filamu zinazotakiwa ni kama zifuatazo:
• Filamu inayoelezea story kuhusu muziki ama wanamuziki wa bara la Africa ama waafrika waliopo ng’ambo (diaspora)
• Filamu inayowakilisha utajiri na mchanganyiko wa muziki wa Afrika Mashariki na zaidi
•Filamu za muziki zitakazowavutia wakazi wa nyumbani na watazamaji wa kimataifa
• Filamu zenye picha nzuri, sauti zenye ubora na muziki wenye chimbuko la Africa.
• Filamu ambazo zina sauti mpya na ambazo hazijawahi kusikika pamoja na wasanii waliofanikiwa
• Filamu zenye lugha ngeni zinatakiwa kuwekewa subtitles za Kiswahili na Kiingereza
Kwa wale ambao wangependa kushiriki fomu zipo kwenye website ya Sauti za Busara, busaramusic.org. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 16, November 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents