Habari

Scarlett Johanssen kuwa muigizaji wa kike anayelipwa pesa nyingi zaidi


Muigizaji na mrembo Scarlett Johansson ataweka mfukoni kiasi cha paundi milioni 13 kwa kuigiza kwenye filamu ya Avengers 2.
Kiasi hicho hakijawahi kulipwa kwa muigizaji yoyote wa kike duniani kwaajili ya kuigiza movie.
Malipo hayo ya paundi milioni 13 yanamwondoa Angelina Jolie kama muigizaji wa kike aliyewahi kulipwa pesa nyingi zaidi kwa kuigiza movie moja tu ambapo alilipwa paundi milioni 12.2 kuigiza kwenye filamu ya The Tourist.
Mabosi wa filamu hiyo wanataka Scarlett asaini deal hilo baada ya filamu ya Avengers ya kwanza kukusanya zaidi ya paundi milioni 936 na hivyo kushika nafasi ya tatu kwenye historia ya filamu zilizouza zaidi duniani nyuma ya Avatar na Titanic.
Chanzo kimoja kimesema: “Scarlett ni muigizaji hot kwenye Hollywood na uwepo wake kwenye muendelezo wa filamu hiyo ni wa lazima.”
“Watayarishaji wanadhani kuwa akiwa kama mwanamke anayeongoza kwenye filamu hiyo,mashabiki wake kiume humuona kama kiungo muhimu kwa urembo wake na jinsi anavyofit kwenye story. Anapendwa na wachambuzi wa filamu pia.”
“Kila mtu anaamini kuwa atasaini na kuwa tayari kwa kuanza kushoot mwaka 2013.”
Robert Downey Jr, Chris Hemsworth na Jeremy Renner wanatarajia kuongezewa asilimia 50 ya malipo pia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents