Habari

Scorpion ‘mtoboa macho’ ahukumiwa miaka 7 jela na faini ya tsh milioni 30

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu, Salum Njwete maarufu Scorpion miaka 7 jela kwa kosa la kumjeruhi na kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho, pia mahakama imemtaka kulipa faini ya TSH. Milioni 30 kwa ajili ya fidia kwa majeruhi huyo.

Kwa upande wake, mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni majeruhi, Said Mrisho amelia mahakamani hapo akidai adhabu aliyopewa Scorpion haitoshi ikilinganishwa na kosa alilotenda huku akieleza kuwa atakwenda kwa Rais Dkt. John Magufuli kumueleza masikitiko yake.

Njwete anlikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka jana katika eneo la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam. Pia, anadaiwa kumwibia mali yenye thamani ya Sh 476,000/-

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents