Habari

Sean Kingston Kutua Leo Usiku

Msanii mwenye asili ya kijamaica mwenye makazi yake jijini Miami Sean Kingston anatarajiwa kuwasili leo usiku akitokea nchini Marekani.

Kwa mujibu wa habari ambazo bongo5 imezipata Sean Kingston anakuja moja kwa moja Tanzania kama mgeni mwalikwa wa Tunzo za Kilimanjaro Music Awards na pia kama mtoa burudani katika tamasha litalojumuisha washindi wa tunzo hizo zinazotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Usikuwa tarehe 14 na Jumamosi jioni ya tarehe 15.

Katika Ujumbe wake wa Kuwaaga mashabiki, Sean Kingston amewaambia kuwa anasafiri kuja Tanzania Africa na anategemea kufanya show kali na kabambe.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo eenie Meenie alikuwa jijini Amsterdam mida ya Asubuhi ya leo anatarajiwa kuwasili na Dj wake maarufu Dj Hype King pamoja na baadhi ya washkaji wake wa kundi linalojiita “time is Money” tukimnukuu Sean Kingston anasema AFRICA”” GET READY cuz THE TIME IS MONEY BOYZ IS COMING AND WE GOING INNN!!! POW POW!!!

Bongo5 itakupa habari zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents