Burudani

Sebastian Maganga aeleza A-Z afya ya Ruge Mutahaba, amtaja Rais Magufuli

Moja ya viongozi wa juu wa Clouds Media Group, Sebastian Maganga amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu afya ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge Mutahaba.

Image result for ruge mutahaba
Ruge Mutahaba

Sebastiani akiongea katika kipindi cha Clouds 360 amesema kuwa kuanzia mwezi May hadi June mwaka huu, hali ya afya ya Ruge ilikuwa mbaya jambo ambalo lilipelekea Ofisi impumzishe kwa muda.

Ni kweli mengi yamezungumzwa lakini ukweli halisi ni huu…katikati mwezi wa 5 kulelekea mwezi wa 6 hali ya Mkurugenzi haikuwa nzuri na akatuomba kupata muda kidogo ili ashughulikie afya yake na tuliona hili litakuwa dogo tu na tukatoa baraka zote. Lakini ripoti za kitabibu zikasema muda wa kupumzika ni mdogo hivyo akaongezewa muda na katikati ya mwezi wa 6 na wa 7 alirejea na kasi ya kawaida kwenye kazi na wiki mbili tatu tukawa nae na hapo ndiyo tulikuwa tunakaribia kuanza Tigo Fiesta moro. Akatuambia anabidi aelekee kwenye taratibu za kimatibabu na nikiri bado changamoto hizo zipo na madaktari wanakiri Kiongozi wetu ni mpambanaji na bado anahitaji muda wa kupumzika na ni kweli hizo changanoto zilikuwepo,“amesema Sebastian Maganga.

Maganga amesema taarifa za kuugua kwa Ruge zilimfikia Rais Magufuli, jambo ambalo lilimuumiza na kumfanya achangie mfuko wa afya.

Tunamshukuru Rais kutokana na yeye mara baada ya kupata taarifa hizi alinyoosha mkono kwetu na kutuambia changamoto za kiafya ni kubwa na la awali ambalo anataka kulifanya ni kuchangia mfuko wa kiafya na changamoto zisiwe gharama za kimatibabu na kutoa dola elfu 20,000,“amesema Maganga.

Taarifa hiyo, imekuja baada ya sintofahamu iliyokuwepo kwa takribani wiki mbili kuhusu afya ya Ruge Mutahaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents