Habari

Seki wa Orijino Komedi aliwahi kuwekwa ndani ‘kisa’ kuigiza sauti ya Nyerere

Producer na mastermind wa Orijino Komedi, Sekioni David aka Seki leo amekumbushia namna alivyotoka mbali katika sanaa ya uigizaji wakati kundi lake likisaini mkataba na kampuni ya Nexus Consulting Agency kwenye hoteli ya Serena leo jijini Dar es Salaam.

IMG_4519

Seki ambaye aliwahi kutamba kwenye tamthilia ya Mambo Hayo ya ITV, alikumbushia kuwa mwaka 2000 wakati anaanza sanaa aliwahi kukamatwa na polisi na kulala selo kwa muda baada ya kusikika akiigiliza sauti za hayati Baba wa Taifa, Mwal Julius Nyerere na ile ya rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Polisi walimkamata Seki kwa madai kuwa alikuwa akiwadhalilisha viongozi hao wa Afrika.

Seki alisema hayo baada ya kuonyesha furaha iliyotokana na kundi lake la OK kula shavu nono litakalowapeleka mbali zaidi kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents