Technology

Sekta ya mawasiliano ya simu yenye kampuni chache lakini zenye ubora itakuza uchumi na huduma

Katika muongo uliopita sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania imeshuhudia ukuaji mkubwa na kuongezeka kwa kasi kwa maendeleo ya teknolojia. Katika wakati huu makampuni ya simu yamefanya kazi kubwa kuwapa wateja huduma bora na ubunifu ambao umeleta mabadiliko makubwa ya kidijitali.

Sambamba na hilo, sekta hii pia imekuwa moja ya sekta bunifu zaidi katika bara la Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara hasa katika teknolojia bunifu kwenye kufanya malipo kwa njia ya simu, huduma za bima na afya. Ni muhimu kwamba maendeleo haya yote kwenye sekta hii yawe na tija ya muda mrefu kwenye maisha ya Watanzania. Mfano kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi kumeongeza idadi ya ajira hasa kwa wenye simu janja sio tu kwa watu binafsi lakini hata kwenye biashara na taasisi za kiserikali.

Huku sekta hii ikiendelea kutanuka zaidi, yako mengi ya kufanya ili kuhakikisha inaendelea kuwa juu na kutupa faida zaidi na hakika hatua zimeanza kuchukuliwa za aina mbalimbali ili kuhakikisha hilo. Mfano, Novemba mwaka jana ilitangazwa kuwa Tigo na Zantel wameunganisha huduma zao ili kuongeza nguvu na kuboresha huduma kwa wateja wa kampuni zote mbili. Hatua kama hizo ni muhimu sana.

Wataalamu wa sekta ya mawasiliano wanaweka bayana kuwa kampuni chache zenye ubora sokoni ni bora kwa wateja na taifa kwa ujumla tofauti na kuwa na utiriri wa kampuni lakini zenye huduma zisizo bora. Kampuni zikifanya kazi pamoja kama mfano wa Tigo na Zantel huwekeza vizuri zaidi faida ili kutoa huduma bora na za kibunifu zaidi.

Mwaka 2020 umeanza na tunaelekea kuanza muongo mwingine mpya, tutarajie matunda haya ya siku za karibuni ambayo tumeyaona kwenye sekta ya mawasiliano ya simu kuwa ni mwanzo tu, kwani sekta hii ina mengi makubwa sana ya kutupatia Watanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents