Selah Marley: Mtoto wa Lauryn Hill na Rohan Marley anayetumika kama model kwenye nguo za Beyonce na Kanye West

Kizazi cha hayati Bob Marley kamwe hakitokuja kupotea kwenye tasnia ya burudani.

Wakati ambapo watoto wake hawasikiki sana kwenye muziki mpya, wajukuu zake wanazidi kuja juu. Ni hivi karibuni tu mjukuu wa Bob, Skip Marley – mtoto wa Cedella Marley alishirikishwa kwenye wimbo wa Katy Perry, Chained to the Rhythm.

Lakini wakati muziki ni kitu ambacho watoto na wajukuu wa Marley wanafanya zaidi, mjukuu mwingine ameamua kuingia kwenye fashion na taratibu jina lake limeanza kupenya.

Anaitwa, Selah Marley, binti wa Lauryn Hill na Rohan Marley.

Selah ametumika kama model kwenye nguo za Beyoncé, Ivy Park.

Pia ameshatangaza nguo za Calvin Klein, Chanel na Yeezy, huku pia kwa sasa akijaribu kuingia kwenye muziki.

Tazama picha zake zaidi:

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW