Habari

Selena Gomez akataliwa kuingia Urusi kufanya show kwa sababu ya kuunga mkono haki za mashoga

Selena Gomez ni miongoni mwa watu wanaounga mkono haki za mashoga, na msimamo huo umemcost mpenzi huyo wa zamani wa Justin Bieber na kusababisha anyimwe Visa ya kuingia nchini Urusi alikotarajiwa kufanya maonesho mawili mwezi huu (September).

Selena Gomez

Gomez (21) ambaye ni mwigizaji na mwimbaji alipagwa kufanya show mbili (September 23) na la pili lilipangwa kufanyika (September 25) katika taifa hilo la kikomunist wakati wa ‘Stars Dance tour’ ambayo anazunguka katika nchi mbalimbali, lakini maafisa wa nchi hiyo wamelitupilia mbali ombi lake la kupewa Visa kutokana na kuunga kwake mkono haki za mashoga.

Selena si msanii wa kwanza kukutana na vipingamizi kama hivyo Russia kutokana na misimamo ya kuunga mikono mashoga. Hapo kabla Madonna na Lady Gaga waliwahi kushow love kwa jamii ya mashoga walipofanya show nchini humo mwaka 2012, na baadaye serikali ya nchi hiyo ilitishia kuwashitaki kwa kufanya onesho bila kuwa na nyaraka sahihi za vibali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents