BurudaniVideos

Salif Keita Apamba Dar

Mwanamuziki Nguli kutoka nchini Mali, Afrika ya Magharibi, Selif Keita  mwenye ulemavu wa ngozi, juzi alipanda jukwaani na kupagawisha mashabiki wake katika katika onyesho la aina yake lililofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. (Angalia videos hapa)

Watu wengi walijitokeza na kupata mzuka mwingi hadi  kupiga mayowe ya furaha kwa jinsi mwanamuziki huyo alivyowakamata mashabiki wake ikiwa  ni onyesho lililosisimua sana.

Mwanamuziki Selif Keita anadhihirisha uwezo wake wa kuimba kwa mpangilio wa vyombo vya muziki ukichagizwa na waimbaji wake mahiri ambao walionekana kulitawala jukwaa katika kiwango cha hali ya juu.

Keisha, mwanamuziki  wa hapa nchini ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, alitangulia kupanda jukwaani na kuimba  kwenye onyesho hilo kabla ya msanii huyo mahiri wa Afrika Magharibi kutumbuiza.

Kati ya wageni walioalikwa ni aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Shaymar Kwegyir na wadau mbalimbali wa muziki.

Onyesho hilo lilidhaminiwa na  Benki ya  Stanbic.

{hwdvs-player}id=1206|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1205|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1204|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1203|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1202|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1201|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents