Burudani

Sema Yote: Ommy Dimpoz afunguka kuhusu sehemu ya mali zake na miradi (Audio) Part 1 (Exclusive)

Kwa kutambua kuwa unapenda kujua siri za wasanii wa uwapendao, Bongo5 inakuletea ‘Sema Yote’ aka Tell it All.

4ff716621ac811e3a73722000a1f9317_7
Ommy Dimpoz

Kwa maneno yao wenyewe, sauti zao wenyewe bila kulazimishwa na mtu, wasanii wataeleza siri zao, siri nzuri lakini ambazo hujawahi kuziskia sehemu yoyote, kuanzia mafanikio yao na mali zao, namna walivyofall in love, siri zao za utotoni, ndoto zao na siri zingine kibao.

Angalizo lakini, Sema Yote si kitu cha kila siku, ni kitu cha msimu na hakina muda maalum.

Leo tumemkamata Omar Nyembo aka Ommy Dimpoz ambaye kwa mara ya kwanza anatoa siri nzito, usishtuke sana, siri nzito kuhusu sehemu ya mali alizojikusanyia hadi sasa.

Haya ni miongoni mwa mambo aliyoyaongea kwenye Sema Yote (Tell it All)

Kuhusu sehemu ya mali aliyonayo Ommy Dimpoz

Najenga kwanza nyumba mbili ambapo moja imeshakamilika kwa kiasi fulani na nyingine nayo inaelekea kukamilika. So far project zote mbili hizi tangia nimeanza kujenga ukija kupiga mahesabu ni hela nyingi kidogo inakaribia 250 (milioni tshs) ukiangalia project zote zinavyoenda kwa pamoja sababu ujenzi unakula sana hela ndo maana nakuambia ukitaka kupiga mahesabu unaanza kujiuliza ‘hivi hela zote zikiwa kwa pamoja ni zangu’. Kwahiyo ukiangalia hivyo halafu kuna ununuzi, viwanja, nina viwanja pia viwili. Natarajia pia kuja na project nzuri ya kibiashara ambayo itakuwa na brand yangu kabisa ya PKP (Pozi Kwa Pozi)

Kuhusu hela anayolipwa kwenye show

Milioni nane kwenda juu sababu inategemea, kuna show za makampuni, kuna show za club na lazima niwe na timu yangu pia, dancers wanne na meneja. Kubargain kupo, unaweka kiwango cha show, inategemea sometimes promoter anataka akupe show ngapi, kuna kazi za kuungaungana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents