Michezo

Sepp Blatter na Michel Platini wafungiwa miaka nane na FIFA

Kamati ya maadili ya shirikisho la soka duniani FIFA, imewafungia Sepp Blatter na Michel Platini kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka 8 kufuatia kukutwa na kosa la ubadhilifu wa fedha na kupigwa faini.

article-3368574-2F8B77F800000578-706_964x373

Maamuzi hayo yalitangazwa siku ya Jumatatu mjini Zurich, yamedhihirisha mwisho halisi wa uongozi wa soka kwa Blatter na Platini wote wakiwa hawana uwezo kugombea urais wa FIFA Februari 26.

Chombo cha upelelezi kilipendekeza kuwafungia maisha baada ya kuwepo na taarifa zisizo rasmi za kifedha pauni milioni 1.35 ambazo rais wa FIFA Blatter alimlipia rais wa UEFA Platini miaka tisa baada ya kumaliza kazi yake.

Mashtaka yalithibitishwa ikiwemo kutoa zawadi, mgogoro wa kimaslahi, na kuvunja uaminifu kwa FIFA.

Taarifa ya FIFA ya Jumatatu inasema:

Kamati ya maadili inayoendeshwa na Hans Joachim Eckert imewafungia Joseph S. Blatter, Rais wa FIFA, kwa miaka nane, na Michel Platini na Rais UEFA, kwa miaka nane kujishughulisha na masuala ya soka (uongozi, michezo au mingine yoyote) kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa. Kifungo hiko kitekelezwe haraka.

“Blatter amepigwa faini pauni 33,700, huku Platini akipigwa faini pauni 53,940.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents