Michezo

Serengeti Boys kutupa karata ya kwanza leo Gabon

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inaingia uwanjani hii leo katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Mataifa ya Afrika,ambapo vijana wa Tanzania watapimana ubavu na mabingwa watetezi timu ya Taifa ya Mali, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville nchini Gabon.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime ameuwelezea mchezo wao huku akithibitisha kuwepo kwa mchezaji mmoja ambae ni majeruhi na atakosekana na katika michezo yote ya mashindano hayo, huku akiwatoa hofu watanzania kutokuwa na presha.

Vijana wa Serengeti Boys wataingia uwanjani hii leo huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya matokeo waliyoyapata wakati walipoweka kambi nchini Morocco baada ya kucheza michezo miwili ya kujipima ubavu dhidi ya wenyeji Gabon ambapo katika mchezo wa awali waliweza kufanya vizuri na hata ilipokutana na Cameroon iliweza kuchomoza na ushindi katika mchezo wa kwanza wa goli 1 kwa 0 na mchezo wa marudiano wenyeji Cameron wakarudisha kipigo cha goli 1 kwa 0.

Serengeti Boys waliweka kambi ya mwezi mmoja Rabat nchini Moroco kwa ajili ya kujiandaa na michuano hii mikubwa kabisa barani Africa ambayo tayari imeshaanza na leo kikosi cha Tanzania kitatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Bingwa Mtetezi Mali.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents