Michezo

Serengeti Boys wakiwa katika Mapumziko

Leo, kikosi cha Timu ya Taifa ya vijana chini ya Umri wa miaka 17 “Serengeti Boys”, kimeonekana kikiwa katika Mapumziko.Serengeti Boys itaingia uwanjani May 15 katika Fainali za 12 za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon 2017.

Katika Michuano hiyo mikubwa kabisa kwa Afrika inatarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28 mwaka huu katika miji ya Libreville na Franceville nchini na kila timu itakuwa na wachezaji 21 kikosini.

Mpaka sasa timu nane zimegawanywa katika makundi mawili, A likiundwa na wenyeji Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana na B likiundwa na Mali, Tanzania, Angola na Niger. Timu mbili za juu katika kila kundi zitafzufu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia, ambazo zitafanyika nchini India kuanzia Oktoba 6 hadi 28, mwaka huu.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents