Michezo

Serengeti Boys yatupwa nje CecafaU17

Serengeti Boys wamepoteza mchezo wa nusu fainali ya CECAFA U17 na kuishuhudia Uganda ikifuzu fainali kwenda kucheza na Ethiopia ambao waliifunga Rwanda hapo Jana.

Tanzania imetupwa nje baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Uganda.

Uganda inaingia fainali na itakutana na Ethiopia kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili Agosti 26 kwenye uwanja huo huo.

Magoli ya Uganga yalifungwa na Abdul Idd dakika ya 4, John Alou dakika ya 76, Amiri Njiru dakika za nyoneza huku goli la Serengeti Boys likifungwa na Edson Mshirakandi dakika ya 11.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents