Shinda na SIM Account

Sergio Romero wa Man United kulikosa kombe la dunia mwaka huu

Ndoto za kila mchezaji ambaye timu yake ya taifa imefanikuwa kufuzu kombe la dunia, anahakikisha anacheza michuano hiyo ambayo itafanyika Urusi mwezi Juni mwaka huu.

Hata hivyo baadhi ya wachezaji wameanza kupoteza ndoto hizo akiwemo golikipa wa Manchester United, Sergio Romero ambaye hatakuwepo tena kwenye kikosi cha Argentina kufuatia kuumia goti lake la kulia.

Romero amejitonesha jeraha hilo na wakati alipokuwa akifanya mazoezi na timu hiyo ya taifa.

Nafasi yake kwenye michuano hiyo inatarajiwa kuchukuliwa na Franco Armani wa Atlético River Plate ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu katika ligi kuu ya Argentina.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW