Burudani

Series ya Empire yaendelea kuvunja rekodi ya TV, hujaiona? Unapitwa na mengi!

Umaarufu wa series mpya ya Empire ya kituo cha Fox, unazidi kuwa mkubwa.

https://www.youtube.com/watch?v=dBzu_jKLJek

Series hiyo ambayo haina hata mwezi tangu ianze kuoneshwa imekuwa gumzo si tu Marekani, bali sehemu nyingi duniani.

Kutazamwa kwake kumeizidi series ya ‘How to Get Away With Murder’ ya ABC kama series mpya ya kwanza msimu huu miongoni mwa watazamaji wenye miaka chini ya 50.

https://www.youtube.com/watch?v=0GqsaysflOU

Pamoja na kupendwa na watu wa rangi zote, Empire imeiteka zaidi jamii ya wamarekani weusi ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Nielsen, episode ya wiki iliyopita iliangaliwa na asilimia 33 ya makazi wanayoishi wamarekani weusi hiyo ikiwa ni sawa na mara tano zaidi ya show ya NCIS: Los Angeles.

Mafanikio yake yanaifanya Empire kuwa series mpya iliyoanza kwa mapokezi makubwa zaidi katika kipindi cha miaka 20.

Empire imechezwa na Terrence Howard anayeigiza kama mfanyabiashara wa muziki aitwaye Lucious anayefanikiwa kutoka maisha ya mtaa ya kuuza unga na kuja kumiliki label ya muziki.

Ana watoto watatu Andre, (Trai Byers) ambaye ni mkubwa, Jamal (Jussie Smollett) ambaye pamoja na kuwa ni shoga ni muimbaji mkali balaa ambaye haelewani na baba yake kutokana na hali hiyo na mtoto wake mdogo Hakeem (Bryshere Gray) ambaye amekuwa bila kulelewa vyema na wazazi wake na pia ni rapper.

Pia kuna mama yao, Cookie (Taraji) ambaye anatoka jela kuja kutetea pia mali alizochuma na mume wake Lucious. Cookie ni mhusika anayependwa zaidi kwenye series hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents