Habari

SERIKALI: hakuna aliyejuu ya sheria

SERIKALI imesema hakuna aliye juu ya Sheria na kwamba hata Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, anaweza kuchunguzwa na Polisi kuhusu tuhuma za rushwa.

SERIKALI imesema hakuna aliye juu ya Sheria na kwamba hata Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, anaweza kuchunguzwa na Polisi kuhusu tuhuma za rushwa.


Hata hivyo imesisitiza kuwa suala hilo linapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu na uangalifu mkubwa, kwa kuwa watu wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa wanaweza kumpaka matope kiongozi huyo wa TAKUKURU kwa kuwa ameonekana kuwa mwiba kwao.


Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Mary Nagu, akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu tuhuma zilitolewa kupitia mtandao wa tovuti kuwa Hosea anakabiliwa na tuhuma za rushwa.


Alipoulizwa kama Mkurugenzi huyo ana kinga kikatiba alisema “Kikatiba hajatajwa, bali waliotajwa ni Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu na mawaziri, ila mahitaji ya yeye kutajwa moja kwa moja yalijitokeza ili kuweka ulinzi fulani, lakini bado halijawekwa,” alisema Dk. Nagu


Kauli hii imekuja kama ufafanuzi kuhusiana na kauli nyingine aliyoitoa hivi karibuni Waziri Marmo kuhusiana na tuhuma ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kompyuta dhidi ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, Hosea“.


Akizungumza na gazeti moja kwa simu akiwa nje ya nchi, Marmo alisema Serikali inachunguza tuhuma hizo ili kuona ukweli na uhalali wake, huku aliyetuhumiwa akikanusha madai yaliyotolewa katika mtandao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents