Habari

Serikali kuboresha posho kwa Maaskari

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi amesema kuwa serikali itendelea kuboresha posho ya chakula na posho kwa Maafisha na Maaskari kadri uwezo wa serikali utakavyo ruhusu.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi

Dkt Mwinyi ameyasema hayo leo, Wakati akijibu swali la mbunge Haji Khatib Kahi alietaka kujua Lini serikali itaongeza posho la Maafisa na Maaskari ili iendane na maisha?

“Jeshi la ulinzi la Tanzania linafanya kazi zake kwa kuwapatia Maafisa na Maaskari posho za aina mbalimbali. Serikali imekuwa ikiboresha maslahi na stahiki mbalimbali kwa Maafisa na Maaskari kwa kuzingatia hali ya maisha ya wakati husika na uwezo wa serikali kifedha kumudu kulipa stahiki hizo, racial alliance inalipwa kwa Maaskari na Maafisa wote,” alisema Dkt Mwinyi.

“Serikali ilipandisha kwa nyakati tofauti kwa mfano mwaka 2011 racial alliance ilikuwa 7500 mwaka 2014 ilipanda kufikia 8500 na mwaka 2015 ilipandishwa kufikia 10000 ni kiasi kinaendelea kutolewa hadi hivi, kwahivyo serikali itaendelea kuboresha posho ya chakula na posho nyinginezo kadri uwezo wa serikali utakavyo ruhusu.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents