Habari

Serikali kuendelea kuwawezesha wenye ulemavu (+Video)

Serikali imewahakikishia watu wenye ulemavu kwamba itaendelea kuwawezesha kwa namna mbali mbali ili wawaze kutoa mchango wao katika maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Stella Ikupa, wakati akifungua mafunzo ya Usalama na Afya yaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa watu wenye ulemavu Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Ikupa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inatambua mchango mkubwa wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii hivyo itaendelea kuliwezesha kundi hilo kwa kuweka mazingira rafiki ya uzalishaji kupitia Taasisi zake ikiwemo OSHA.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Taasisi yake wa kuyafikia makundi mbali mbali katika jamii na kutoa mafunzo ya Usalama
na Afya yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa kuzingatia kanuni za afya na usalama.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza OSHA kwa kuwapa mafunzo na kutoa wito kwa Mamlaka hiyo kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa makundi mbali mbali wakiwemo watu wenye ulemavu kwa nchi nzima.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents