Habari

Serikali kufadhili miradi ya kuinusuru Zanzibar na mabadiliko ya tabia nchi

Serikali, kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema itafadhili miradi mingi zaidi ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa upande wa Zanzibar.

Waziri Makamba akikagua maendeleo ya miradi hiyo visiwani Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba leo ijumaa tarehe 20 Oktoba 2017, wakati akikagua miradi miwili ya uhifadhi wa mazingira inayofadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais inayofanywa visiwani  Zanzibar.

Waziri Makamba amesema kwamba Zanzibar, kutokana na kuwa kisiwa, iko hatarini zaidi na kuinuka kwa kina cha bahari kunakotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Tayari Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza miradi ya aina hiyo katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa pwani ikiwemo Bagamoyo, Dar es Salaam, Pangani, Rufiji, Pemba na Unguja.

Mhe. Makamba leo amekagua mradi wa ujenzi wa kuta za bahari zinazojengwa eneo la Kilimani ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Ujenzi wa kuta hizo utagharimu zaidi ya Dola $300,000 sawa na Tsh milioni 674 na tayari ujenzi umeanza tarehe 25 Julai mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.

Uamuzi wa upandaji wa mikoko na ujenzi wa kuta hizi ulifikiwa ili kupunguza maji ya bahari yanayoingia kwenye makazi ya watu na kupunguza athari za mawimbi ya maji ya bahari kutokana na kupanda kwa kina cha bahari.

Baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi visiwani Zanzibar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents