Habari

Serikali kufungia uuzwaji wa pombe siku za wiki

Serikali nchini Zimbabwe inatarajia kufungia uuzwaji wa pombe kwa siku za wiki ili kuimarisha afya za wananchi na kuongeza ufanisi kwenye kazi za uzalishaji.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Mail la Zimbabwe, tayari, kamati ya baraza la mawaziri limeidhinisha muswada wa sheria ya kupiga vita ya uuzaji wa bidhaa za pombe wakati wa siku za wiki (Jumatatu- Ijumaa) na kuzuia kabisa  wanawake wajawazito vinywaji hivyo.

Waziri wa zamani wa afya wa Zimbabwe, Timothy Stamps, ambaye pia ni mshauri wa Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais na Baraza la Mawaziri, amependekeza muswada huo ujadiliwe haraka bungeni ili sheria iweze kupitizwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa AFK Insider Zimbabwe inatajwa kuwa ni nchi ya 14 barani Afrika kwa utumiaji wa pombe ambapo mtu mmoja hutumia wastani wa lita 5.1 kwa mwaka.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents