Habari

Serikali kusambaza umeme vijiji vyote

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo Jumanne jioni alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu,”alisema Waziri Mkuu.

“Lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.”

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Lindi Mhandisi, Johnson Mwigune Kwa upande wake, alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu mkandarasi aliyepangiwa katika vijiji hivyo atakuwa tayari ameanza kazi ya kusambaza umeme.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents