Habari

Serikali kuwapima wanaume UKIMWI na TB hata wakiwa Bar

Serikali imesema katika mikakati yake ya kuwatambua wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na TB wameazimia kutembelea maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo baa, migodini na maeneo ili kuwafikia kirahisi hususani wanaume.

Hayo yameelezwa leo Aprili 23, 2018 Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara Afya, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.

Dkt. Ndugulile alisema mara baada ya serikali kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI, waliamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari.

“Lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza tumetengeneza mikakati jumuishi kati ya ugonjwa wa TB na UKIMWI”, amesema Dkt. Ndugulile.

“Sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo lipo kwenye mikakati ya serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents