Habari

Serikali kuwashughulikia waliohusika kumchapa viboko mwanamke hadharani mkoani Mara

Siku ya jana kuna video iliyosambaa ikimuonyesha mwanamke akichapwa viboko hadharani iliyobabisha hasira miongoni mwa watu wengi. Na sasa, serikali imeviagiza vyombo vyake vya kiuchunguzi kufuatilia chanzo chake.

Kwenye video hiyo, anaonekana mwanamke akichapwa viboko mbele ya mkutano na kuahidi ndani ya muda mfupi itatoa taarifa rasmi huku ikisema haitasita kutoa adhabu kali kwa yeyote aliyehusika.

https://youtu.be/HxrXzWO3umM

Akizungumza ofisini kwake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema amechukizwa na kitendo hicho cha ukatili dhidi ya wanawake huku akisema vitendo hivyo havikubaliki.

“Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na dhidi ya mtu yeyote yule havikubaliki, na ni kosa kwa mujibu wa sheria na ndio maana nimeahidi kwamba tutaendelea kufuatilia suala hili mpaka tuwabaini wahusika ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

“Kauli yetu, vitendo hivi havikubaliki na tutachukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote yule ama kikundi chochote kile, ama mamlaka yeyote ile ya kimila ama ya kibinadamu huko ilipo kama haitofuata sheria na kama haitoelekeza ukatili dhidi ya kundi lolote lile au mtu yeyote yule atachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Kigwangalla.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents