Habari

Serikali: Misaada yote itawafikia waathirika wa tetemeko la ardhi

Waziri mkuu Kassimu Majaliwa amewahakikishia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kuwa serikali ipo makini katika kuratibu misaada inatolewa kwaajili yao na kwamba itawafikishia misaada waathirika wote bila ubaguzi.

majaliwapicha

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo wakati akipokea msaada wa jumla ya shilingi bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi.

“Nataka niwahakikishie watanzania kwamba michango hii ambayo tunaipokea ya fedha na vifaa mbalimbali vya ujenzi pamoja na vyakula tunaendelea kuvipeleka Bukoba vyote,tuna kamati moja tu inayoshughulikia ugawaji na kamati hiyo iko Kagera,” alisema Majaliwa.

Kwa upande mwingine alitoa ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watu na waathirika wa tetemeko hilo kuwa misaada haiwafikii.

“Kunaweza kutokea malalamiko kwamba wengine hawajafikiwa, lakini nataka niwahakikishie waathirika wote wanatambulika kwasababu walisharatibiwa na kamati za maafa za wilaya, tutawafikia wote,” alifafanua.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents