Burudani

Serikali Nigeria yaufungia wimbo wa ‘This is Nigeria’ wa rapa FALZ, masuala ya uchochezi na kidini yatajwa mwenyewe ageuka mbogo

Serikali nchini Nigeria imetangaza kuufungia wimbo wa ‘this is Nigeria’ wa Rapper FALZ kwa kile walichodai kuwa unahatarisha usalama na umekaa kichochezi.

Barua hiyo ya kuufungia wimbo huo iliyotolewa na  Tume ya Taifa ya Utangazaji ya nchini humo (NBC) imetaja baadhi ya mashairi ya wimbo huo kuwa yamelenga kuchafua serikali iliyopo madarakani kama “Hii ndio Nigeria nchi ambayo kila mtu ni mhalifu”.

Hata hivyo winbo huo umefungiwa kupigwa kwenye vituo vya Runinga na Radio pekee, mpaka sasa wimbo huo wenye miezi mitatu mtandaoni umetazamwa mara milioni 13 .

Wimbo wa ‘This Is Nigeria’ ni parody ya wimbo wa ‘This is America’ wa Childish Gambino kutoka Marekani. Wimbo huo wa This Ids Nigeria ulipokelewa kwa mitazamo tofauti tofauti ikiwemo rapa P. Diddy ambaye aliupokea kwa mikono miwili kwani alisema ni wimbo ambao unaweza kubadilisha jamii kutoka kwenye mawazo hasi hadi chanya.

SOMA NA HII – Waislamu Nigeria wamjia juu rapa Falz, wampa siku 7 afute video ya wimbo wake mpya ‘This is Nigeria’

Mapema mwezi Mei mwaka huu Waislamu nchini Nigeria walitoa onyo kwa rapa Falz kuwa aufute wimbo huo kwa madai kwamba video ya wimbo huo inadhalilisha waislamu nchini humo jambo ambalo Menejimenti ya FALZ iligoma kufuta video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents