Serikali Vs Madereva wa Daladala.

dala dala_m.jpgSerikali imesema inatarajia kuongeza nauli ya magari ya abiria nchini ikiwamo daladala zinazotoa huduma jijini Dar es Salaam, mara tu baada ya Bajeti ya Serikali kutangazwa.

Serikali imesema inatarajia kuongeza nauli ya magari ya abiria nchini ikiwamo daladala zinazotoa huduma jijini Dar es Salaam, mara tu baada ya Bajeti ya Serikali kutangazwa.

Aliyasema hayo Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray, jana kwenye mkutano na waandishi wa habari aliouitisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kuzungumzia tishio la madereva wa daladala kugoma kutoa huduma kuanzia Jumatatu.

Mziray alisema Sumatra imeshapopokea maoni ya Wamiliki wa Mabasi ya Abiria mkoani Dar es Salaam (Darcoboa) ya kutaka nauli ya daladala iongezwe na kwamba inachambua maoni hayo ili kuleta uwiano wa kupanda kwa nauli hiyo na gharama za maisha ya wakazi.

Inadaiwa mara tu baada ya kukamilisha uchambuzi wa maoni hayo, Sumatra itatangaza nauli mpya baada ya kujiridhisha kuwa haitawapa mzigo wamiliki na wafanyakazi wa magari ya abiria na abiria.

Aliwataka wamiliki wa magari ya abiria mkoani Dar es Salaam kuvuta subira na kuipa muda Sumatra kukamilisha kazi yake ya kuongeza nauli kama wanavyodai.

Alibainisha kuwa ingawa mapendekezo ya Darcoboa ni kupandisha nauli hiyo kwa asilimia 15, Sumatra itaiangalia upya na kuipitia kwa makini kabla ya kuidhinisha ianze kutumika.

“Tumeyapokea Maombi ya Darcoboa kutaka kuongeza nauli ya daladala na sasa tunayafanyia kazi, Tukiwa na matarajio ya kutangaza nauli hizo mpya baada ya kuona mwelekeo wa bajeti ya mwaka 2008/2009,

“Mziray. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro naye amesema serikali, itawafutia leseni madereva wa daladala watakaogoma kutoa huduma siku ya Jumatatu ili kuishinikiza Sumatra kupandisha nauli.

”Mimi binafsi nawataka waache kabisa, kwani baada ya taarifa hiyo serikali itachukua hatua kuhakikisha kuwa usalama wa madereva na wote watakaoshiriki mgomo huo, watafutiwa leseni,

”alisema Kandoro. Aliendelea kusema “Kupandisha nauli kuna utaratibu wake ambao tayari umeshafanywa na Dacoboa kwa kupeleka mapendekezo yao SUMATRA hivyo madereva wanatakiwa kusubiri uamuzi wa Sumatra”

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents