Michezo

Serikali ya Gabon yaifuta timu ya Taifa, Baada ya kushindwa kufuzu AFCON 2019 ‘hawajitumi, wanajali pesa kuliko uzalendo’

Serikali nchini Gabon kupitia Wizara ya Habari, imetangaza kuifuta rasmi timu ya Taifa ya Mpira wa miguu ya wakubwa, kwa kosa la kushindwa kufuzu AFCON 2019.

Image result for gabon national team

Akitoa tamko la kufuta timu hiyo, Waziri wa Michezo nchini humo, Alain Claude Billie-By-Nze amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo hawajitumi na wameweka maslahi ya pesa mbele kuliko uzalendo.

Tunakwenda kuijenga upya timu yetu ya Taifa kwa misingi bora, tutawaweka pembeni wachezaji wote waliokosa uzalendo na utaifa na wanaoweka pesa mbele. Haiwezekani wachezaji hawajitumi na wanacheza kama wamelazimishwa uwanjani.“amefunguka Waziri Alain Claude Billie-By-Nze.

Watu wengi nchini Gabon wamekuwa wakimshushia lawama mshambuliaji wa timu hiyo ya Taifa ambaye anakipiga katika klabu ya Arsenal, Pierre Aubameyang , kuwa hajitumi uwanjani na amekuwa akijitenga na wachezaji wenzake licha ya mara kadhaa kuisaidia timu hiyo kifedha.

Hata hivyo, Waziri Billie-By-Nze hakufumbia macho tuhuma hizo kwani akiongea na waandishi wa habari jana Machi 27, 2019 alitupa kijembe kwa kusema “Watu wanaojiweka mbele kufadhili timu kifedha na hata kiushauri kwa namna nyingine hatuwezi kuwaita tena,“.

Katika tamko hilo pia ametangaza kuifuta timu ya Taifa ya wachezaji walio chini ya miaka 23 (U-23), na amesema itaundwa upya baadae kwani baadhi ya wachezaji watachukuliwa katika timu ya wakubwa.

Waziri Alain Claude Billie-By-Nze amesema kuwa timu nyingine mpya itatangazwa baada ya siku 60 kuanzia jana ambayo itachukua wachezaji wapya na kocha mpya ambao wote wataweka uzalendo mbele.

Gabon imeshindwa kufuzu AFCON 2019 kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Burundi kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi, ambapo Gabon walikuwa wanahitaji ushindi ili kufuzu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents