Habari

Serikali ya Rwanda yatoa sababu ya kuwataka wananchi wake, wanaofanya biashara mpakani mwa Burundi kuacha mara moja

Serikali ya Rwanda imewasihi wananchi wake walioko karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na nchi ya Burundi kusitisha biashara yoyote na majirani zao wa nchi ya Burundi.Ni siku chache baada ya Rwanda kuwakataza wananchi wake kwenda nchini Uganda.Rwanda inashutumu nchi hizo kusaidia makundi ya waasi yanayoipinga, anaripoti mwandishi wa BBC ,Yves Bucyana.

Kwa mujibu wa BBC. Wito wa kuwakataza wanchi wa maeneo ya mpaka baina ya Rwanda na Burundi kutokwenda nchini humo umetolewa na afisa katika jeshi la Rwanda Jenerali Mbarac Muganga wakati wa mkutano wa usalama baina yake ,wananchi na viongozi wa maeneo ya mpakani upande wa kusini mashariki.Jenerali Muganga amewataka kusitisha shghuli zote zinazoweza kuwalazimisha kwenda nchini Burundi hata kama itakuwa ni kuoa au kuolewa na mtu kutoka upande wa pili:

”majirani wale walituchimbia shimo,kila mnyarwanda anayekwenda huko anatupwa ndani,hii ni kwa mjibu wa taarifa za uhakika tulizo nazo. Hatutawashambulia nchini mwao kwani sisi tunalinda mipaka yetu.Rwanda tunajitosheleza kwa chakula ndiyo maana tunawasihi kutumia kile kidogo tulicho nacho.kuna wengi pia wanaokwenda kuowa au kuolewa upande wa pili wa mpakani si kwamba tunataka kuvunja ndoa zenu lakini tunawasihi kusitisha safari za kwenda huko na vile vile kupunguza wageni mnaopokea kutoka huko kwa sababu wanakuja wakiwa na malengo mengine mengi” .

Burundi imeishaitangaza Rwanda kama adui wake mkubwa.Nchi mbili zinashutumiana kuunga mkono makundi ya waasi kutoka kila upande.Miaka 3 iliyopita Burundi ilitangaza kusitisha biashara yake na Rwanda hasa mboga na matunda na pia kusitisha misafara ya mabasi ya abiria kutoka Rwanda.

Rwanda imekuwa na tahadhari kubwa kwenye mipaka yake kutokana na makundi mbali mbali ya waasi yanayotishia kuishambulia.

Hayo yamejiri wakati ambapo Rwanda iliwakataza wananchi wake kwenda nchini Uganda,nchi iliyokuwa na biashara kubwa na Rwanda.Serikali ilishutumu Uganda kuwanyanyasa wananchi wake wanaokwenda ama kuishi nchini Uganda na pia kusaidia makundi ya waasi wanaotaka kuangusha utawala wa rais Paul Kagame.

By Ally Juma.


Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents