Siasa

Serikali yaahidi haya kwa Shirika la nyumba nchini (NHC)

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula amesema kuwa Shirika la Nyumba nchini(NHC) limeweka mkakati wa kuhakikisha nyumba zote zilizo katika hali ya uchakavu zinafanyiwa ukarabati mkubwa.

Naibu waziri huyo ameyasema hayo Jumatatno hii bungeni, mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Savelina Silvanus Mwijage, lililohoji

nyumba za shirika la nyumba nchini (NHC) ni za muda mrefu na zimekuwa chakavu sana na nyingine zimeanza kubomoka,” Je, ni lini serikali itafanya operesheni kubaini uharibifu uliopo kwenye nyumba hizo?.

“Shirika la Nyumba la Taifa limeshafanya uhakiki wa nyumba zake zote na kubaini hali halisi ya kila nyumba na kuweka mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba hizo kwa awamu. Katika mwaka wa fedha 2016/2017 shirika lilitenga takribani bilioni 11 kwaajili ya kuzifanyia ukarabati nyumba zake ambazo hadi mwezi Machi 2017 jumla ya nyumba 2451 zilikuwa zimefanyiwa ukarabati mkubwa kupitia bajeti hiyo.”

“Aidha idadi ya nyumba zilizofanyiwa ukarabati mkubwa inatarajia kuongezeka ifikapo mwezi Juni 2017, shirika linatarajia kuzifanyia nyumba zote katika mwaka wa fedha 2017/2018 hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa matengenezo ya nyumba ni kazi endelevu kwa shirika hivyo bajeti ya matengenezo itaendelea kutengwa kila mwaka ili wapangaji wa nyumba za shirika waendelee kukaa nyumba zilizo na mazingira bora,” aliongeza Naibu Mabula.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents