Habari

Serikali yadai tatizo la sukari litakuwa historia

Upungufu wa sukari nchini limekuwa ni tatizo kubwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa ambalo Mhe rais John Magufuli pamoja na serikali yake wanaendelea kupambana nalo kuhakikisha mambo yanakaa sawa.

Nyumbna

Kupitia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kinachofanyika bungeni kila siku ya Alhamisi asubuhi, serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim amesema kuwa huu ndiyo wakati mzuri sasa wa kuweka mkakati wa namna sukari inavyoweza kuzalisha na kutosheleza mahitaji ya ndani.

Akijibu Swali la kiongozi wa kambi upinzani bungeni, Freeman Mbowe kumtaka Waziri Mkuu aeleze ni lini sukari ya ziada iliyoagiziwa itawasili nchini ili kuziba pengo la uhaba wa sukari lililopo nchini kwa sasa.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema, “Mwenyewe nimekaa na wamiliki wa viwanda vya sukari tumekubaliana kwa miaka minne wanaweza kuongeza uzalishaji kufikia tani laki nne na ishirini ambazo zinahitajika nchini.”

Aidha Waziri Mkuu amefafanua kuwa “bado tuna maeneo mengi ya uwekezaji wa sukari na mpaka sasa tuna mashamba matatu; Bagamoyo, Morogoro Kidunda, na Kigoma.”

“Lakini lipo eneo jingine pale Kilombero linafaa kabisa kuwekwa viwanda na tayari tumepata wawekezaji ambao wameonyesha nia, kwahiyo sasa tunafanya mazungumzo ya mwisho tuamue kuongeza viwanda ili viweze kuzalisha sukari iweze kufikia mahitaji. Tunajua idadi ya watu inaongezeka na mahitaji makubwa lakini hiyo bodi ya sukari inaendelea kufanya utafiti na inaendelea kuratibu,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents