Habari

Serikali yaeleza hatua iliyofikiwa ya uhakiki wa wafanyakazi

Serikali imesema uhakiki wa watumishi wa umma, utakamilika ndani ya mwezi huu, hivyo nafasi zilizoachwa wazi baada ya kuondolewa kwa watumishi hewa, zitaanza kujazwa.

pichaaa

Akizungumza katika awamu ya pili ya kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa TBC 1 , katibu mkuu ofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema uhakiki wa watumishi hewa, umesaidia kuongeza ufanisi katika taasisi zake.

“Kwa mfano, yupo mtu anatumia majina matatu lakini akatokea mmoja akaondoa lile la katikati na kubaki na majina mawili labda Laurean Ndumbaro hivyo mfumo utaona kuwa ni jina jipya kumbe kuna mtu ambaye amejitengenezea jina hilo,” alisema Dk Ndumbaro.

“Kauli ya Rais ya ‘Hapa Kazi Tu’ inatekelezwa vizuri katika utumishi wa umma. Majukumu yetu ni kuandaa na kusimamia sera, kanuni, taratibu, sheria miundo na miongozo inayohusu rasilimali watu katika watumishi wa umma. Pia jukumu la kusimamia maadili ya utumishi wa umma hasa wale ambao hawaangukii kwenye tume ya maadili ambao sio viongozi wa juu,’’ alifafanua.

Aidha, imesema kwamba baada ya uhakiki huo ambao utasaidia kuwa na orodha sahihi ya watumishi waliopo katika taasisi za umma kwa lengo la kuboresha hali ya utumishi nchini, itaanza mfumo wa kuhakiki majina mapya.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents