Habari

Serikali yaeleza jitihada za kuwawezesha vijana kujikwamua kibiashara

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda imesema kuwa zipo idara nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kujikwamua ili kuendeleza biashara kama kujiunga katika idara ya vijana kwenye Halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa na Kakunda leo, Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Zainab Katimba, aliyehoji “Kwa kuwa jitihada za kutoa mitaji kwa vijana na wanawake inabidi ziende sambamba na kuwajengea uwezo wa kuanzisha na kuendeleza biashara, Je serikali ina mkakati gani wa kuwatumia hawa maafisa Biashara katika kuwajengea uwezo vijana wanaokuwa katika vikundi ambao wananufaika na asilimia 10 inayotengwa kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri?

“Nataka nikuhakikishie kwamba vijana katika nchi hii wana idara nyingi sana za kuweza kuwasaidia mawazo ya kujikwamua kutoka pale walipo kutoka kwenda mbele, kuna idara ya vijana katika Halmashauri kuna idara katika maendeleo ya jamii, kuna idara ya mipango sasa Maafisa Biashara tunawaongezea sehemu nyingine,” amesema Kakunda.

“Kwahiyo mimi napenda nitumie nafasi hii kuwaomba vijana wa nchi hii kutumia fursa ambazo zipo katika Halmashauri wamekuwa hawazitumii ipasavyo, ukienda katika Halmashauri unaona maombi ya vijana yako asilimia 10 ya maombi yote yaliyowasilishwa naomba tujitahidi sisi Wabunge kuwaelimisha kuwaomba vijana wajitokeze katika vikundi na watumie fursa zilizopo kwaajili ya kujiendeleza na serikali tuko macho kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents