Habari

Serikali yaeleza sababu za kushindwa kesi Mahakamani

Serikali kupitia Wizara ya Katibu na Sheria imesema ni kweli kuna baadhi ya kesi ambazo serikali inashindwa kutokana na sababu zinazo sababishwa na serikali kushindwa baadhi ya mashauri pamoja na ushahidi unavyokusanywa na vyombo vya serikali.

Akijibu kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria,leo bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Aida Joseph Kenani mbunge wa Viti Maalum aliehoji

Mara kwa mara serikali imekuwa ikishindwa kesi mbalimbali Mahakamani, Je, Serikali imefanya uchunguzi na kujua sababu za kushindwa kwa kesi mara kwa mara?

“Kama takwimu zinavyoonyesha si kweli imekuwa ikishindwa kesi mara kwa mara, hata hivyo katika nchi yoyote inayozingatia uhuru wa Mahakama na utawala wa sheria serikali haiwezi kushinda kila shauri hata kama haistahili,” alisema Mavunde.

“Ni kweli kuna baadhi ya kesi ambazo serikali inashindwa sababu zinazo sababishwa serikali kushindwa baadhi ya mashauri ni pamoja na ushahidi unavyokusanywa na vyombo vya serikali, kutopatikana kwa mashahidi muhimu, mashahidi kutotoa mshahidi uliotegemewa, baada ya taasisi na mashirika ya umma na idara za serikali kutoshirikisha mapema ofisi za mwanazsheria mkuu zinapofungua au kufunguliwa mashauri Mahakamani namna ushahidi unavyochukuliwa Mahakamani, mashahidi kula njama na kutoa ushahidi unaoathiri mashauri ya serikali.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents