Habari

Serikali yafuta hati za viwanja 5 Muingereza aliyeghushi nyaraka za uraia

Serikali imefuta hati ya viwanja 5 vya raia wa Uingereza aliyegushi nyaraka ilhali mkataba wake wa kuishi unaisha mwakani.

lukuvi-photo1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Akizungumza na ITV Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema, “Tunafuta hati ya kiwanja kwa kupata hizi title, sasa leo tunafuta lakini tumemkabidhi Takukuru wamkamate kwasababu amemiliki kwa taarifa za uongo na tunacho kitambulisho chake kinachoonyesha kwamba yeye sio raia wa Tanzania ni raia wa Uingereza.”

Ameongeza, “Sasa watu kama hawa tunawajua sasa nawapa tahadhari wizara yangu kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali kuwa kamata hawa ambao wamemiliki ardhi yetu ya Tanzania kwa uongo uongo na udanganyifu. Sisi hati hizi tano tumezifuta kuanzia leo.”

Hivi karibuni Lukuvi amekuwa akitatua migogoro ya ardhi sehemu mbalimbali nchini.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents