Habari

Serikali yajipanga kununua korosho, magari ya jeshi yaandaliwa kubeba endapo wanunuzi hawatatii agizo 

Rais Magufuli leo tarehe 10 Novemba, 2018 amekagua magari ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyoandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho za wakulima endapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ifikapo Jumatatu tarehe 12 Novemba, 2018 saa 10:00 jioni.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi amefanya ukaguzi huo katika Kambi ya Jeshi ya Twalipo, Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Mgulani Jijini Dar es Salaam ambapo magari 75 yenye uwezo wa kubeba tani 1,500 kwa mpigo yameandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Tanga.

“Nataka kuwahakikishia wakulima wa korosho Serikali ipo na itaendelea kuwapigania, ikifika Jumatatu saa 10:00 jioni, hawa wanunuzi binafsi hawajajitokeza na kueleza watanunua tani ngapi, Serikali itanunua korosho zote na fedha za kununulia zipo” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Rais amebainisha kuwa baada ya kununua korosho, Serikali itatafuta soko na korosho nyingine zitabanguliwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo rais Magufuli amesema kuwa Serikali inalazimika kuchukua hatua hizi baada ya wanunuzi binafsi kufanya mgomo wa kununua korosho kwa kusuasua licha ya kufanya nao mazungumzo na kufikia makubaliano tarehe 28 Oktoba, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents