Habari

Serikali yakanusha taarifa ya uhaba wa dawa muhimu

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa iliyotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ‘Sikika’iliyosema kuwa kuna upungufu wa dawa muhimu katika hospitali za serikali. Na sasa wizara ya Afya imekanusha taarifa hiyo.

hhhhhhhhhhh

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu hii, waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema taarifa hizo zililenga kuwatia hofu wananchi.

“Taarifa hizi kwa kiasi kikubwa, sio sahihi na sio za kweli,zimetolewa na taasisi moja isiyo ya kiserikali na baadhi ya wanasiasa,” alisema Mwalimu.

“Napenda kuwahakikishia wanahabari suala la afya ni suala la kipaumbele ya serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli,na sisi ambao tumepewa dhamana ya kusimamia sekta hii tunao wajibu wa kuhakikisha tunavyo vifaa tiba vya kutosha,”aliongeza.

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents