Habari

Serikali Yala Sahani Moja Na Richmond

Serikali imefungua uwanja mpya wa mapambano dhidi ya wabunge baada ya kutangaza wazi kwamba ina mpango wa kununua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans, uamuzi ambao unapingwa vikali na wawakilishi hao wa wananchi.

Serikali imefungua uwanja mpya wa mapambano dhidi ya wabunge baada ya kutangaza wazi kwamba ina mpango wa kununua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans, uamuzi ambao unapingwa vikali na wawakilishi hao wa wananchi.

Dalili za kuibuka kwa mapambano kati ya watunga sheria na watawala, zilijidhihirisha jana baada tu ya kubainika kwamba zile tetesi za muda mrefu kuwa serikali ilikuwa na mpango wa kununua mitambo hiyo zilikuwa za kweli, baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuwathibitisha wabunge kuwa mpango huo ni wa kweli.

Mipango ya serikali iliwekwa hadharani jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu msimamo wa kamati yake kuhusiana na suala hilo.

Mara kadhaa gazeti hili limewahi kuandika kuwa kuna mpango wa siri wa serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutaka kununua mitambo ya Dowans, lakini habari hizo zimekuwa zikikanushwa na wahusika au kutotolewa ufafanuzi wa kutosha.

Shelukindo aliweka mambo yote hadharani mbele ya waandishi wa habari kuwa serikali imefikia uamuzi wa kununua mitambo hiyo kwa gharama ya Sh. bilioni 70.

Alieleza kuwa kamati yake juzi iliitwa na Waziri Ngeleja, na kuelezwa uamuzi huo wa serikali na kutakiwa kutoa maoni yake.

Hata hivyo, Shelukindo alisema kamati yake imeieleza wazi serikali kuwa haikubaliani na uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa unakwenda kinyume cha Azimio la Bunge ambalo linataka mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa kampuni ya Richmond ambayo iliiuzia mitambo hiyo Dowans kwanza yatekelezwe kabla ya kufikiwa uamuzi wowote wa kuinunua mitambo hiyo.

“Jana (juzi) kamati iliitwa kwenye kikao cha dharura na Waziri wa Nishati na Madini kuelezwa uamuzi wa serikali kutaka kununua mitambo ya Dowans na tukatakiwa kutoa maoni yetu.

Sisi kama wabunge tumekataa kushirikishwa katika uamuzi huo kwa sababu kwanza kanuni za Bunge haziruhusu jambo lililokwisha pitishwa na Bunge kujadiliwa upya na pili, Sheria ya Manunuzi ya Umma hairuhusu serikali kununua vifaa au mitambo chakavu,“ alisema Shelukindo.

Shelukindo ambaye katika mkutano huo na waandishi wa habari alikuwa amefuatana na mjumbe mmoja wa kamati yake, Christopher Ole Sendeka, alionyesha wazi kukerwa na uamuzi huo wa serikali, ambao alisema ni dharau kwa Bunge.

Alifafanua kuwa moja ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa ikichunguza mkataba wa Richmond ni kutaka watu wote waliohusika kupitisha mkataba huo wachukuliwe hatua za kisheria, lakini kamati yake ikashangazwa kuona kuwa kabla ya hatua hizo kuchukuliwa, serikali imechukua uamuzi wa kutaka kununua mitambo hiyo iliyoleta matatizo makubwa.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents