Habari

Serikali yamsaka Nabii aliyejinadi kuwa anatibu virusi vya Corona – Video

Serikali yamsaka Nabii aliyejinadi kuwa anatibu virusi vya Corona - Video

Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa Serikali imekwishatuma wataalam wake kwa ajili ya kumhoji Nabii namba saba aliyejitokeza na kutangaza kuwa anao uwezo wa kutibu ugonjwa wa homa kali ya mafua inayosababishwa na Virusi vya Corona na iliyopewa jina la COVID-19.

Pichani ni Nabii namba saba aliyetangaza anatibu virusi vya Corona, na Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile

Dkt Ndugulile amesema kuwa endapo watabaini mtu huyo hana utaalamu katika kile alichokitangaza, Serikali itamchukulia hatua stahiki na kuwataka wananchi kuepuka kutoa kauli ambazo zitachanganya jamii.

“Sisi tumeona hizo clip ambazo zinazunguka na sisi tumetuma timu yetu ya wataalam ili huyo bwana akatuthibitishie kama ana uwezo wa kufanya tiba hiyo na atuambie hiyo dawa yake imesajiliwa wapi na yeye amesajiliwa wapi na lini” amesema Dkt Ndugulile.

Hivi karibuni zilisambaa video mbalimbali katika mitandao ya kijamii, zikimuonesha Mosses Mollel, maarufu kama Nabii namba saba, kwamba anao uwezo wa kutibu virusi vya Corona.

Chanzo Eatv,tv

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents