Habari

Serikali yapiga ‘STOP’ matangazo ya uzazi wa mpango kwa muda, waeleza sababu ya kufanya hivyo

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeeleza kuwa imesitisha matangazo yote ya uzazi wa mpango kwenye vyombo vya habari kwa muda, ili kupitia upya matangazo hayo na kujiridhisha kama maudhui au ujumbe unaotolewa kwenye matangazo hayo unaendana na makusudio ya serikali.

Dkt. Faustine Ndugulile

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na kituo cha runinga cha ITV Tanzania.

Kwa upande mwingine, Mhe. Ndungulile amesema kuwa huduma za Afya na Elimu ya Uzazi wa mpango itaendelea kutolewa kama kawaida isipokuwa ni matangazo tu ndio hayatasikika kwenye vyombo vya habari.

Mwanzoni mwa mwezi huu Septemba, Rais Magufuli akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mjini Meatu Mkoani Simiyu, alikaririwa akipingana na masuala ya uzazi wa mpango na kuwataka Watanzania wazaliane bila uoga.

SOMA ZAIDI – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepingana na sera ya serikali yake ya uzazi wa mpango akidai kuwa sera hiyo inapunguza nguvu kazi kwa taifa. 

capture-png.872174

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents