Habari

Serikali yapunguza idadi ya hati chafu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Assad amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea vizuri na uwekaji wa mahesabu uliopelekea kupungua kwa hati chafu katika Taasisi na miradi mbalimbali ya Serikali.

Prof. Assad ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017.

“Katika ukaguzi wa hesabu nilioufanya katika Serikali Kuu na Taasisi zake, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2016/17 nimetoa jumla ya Hati 561 za ukaguzi. Kati ya hati hizo, Hati zinazoridhisha ni 502 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 8, Hati zisizoridhisha ni Saba sawa na asilimia Moja na Hati Mbaya ni Saba sawa na asilimia Moja,” alisema Prof. Assad.

Amesema, katika ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ametoa jumla ya Hati za Ukaguzi 742 ambapo Hati zinazoridhisha ni 697 sawa na asilimia 94, Hati zenye shaka ni 44 sawa na asilimia 5.9 na Hati isiyoridhisha ni moja, Hati hii imetolewa kwa mradi wa maji (WSDP) unaotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Wilaya ya Makete.

Naye, Mjumbe wa Kamati ya LAAC, Mhe. Abdallah Mtolea amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kuonekana kupunguza idadi ya hati chafu na kushamiri kwa hati safi.

Aidha Mhe. Mtolea amesema kuwa kamati hiyo itaziita Halmaushari na kufanya nazo mahojiano bila kuujali matokeo ya ukaguzi kama zilifanya vizuri au vibaya ili kuhakikisha kuna kuwa matumizi mazuri ya fedha za umma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents