Habari

Serikali yataja nchi unazoweza kusafiri bila viza

By  | 

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa zipo nchi 67 ambazo Watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema hayo leo bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.

Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi lililohoji

Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwepo Dimplomasia ya mahusiano, Je ni nchi ngapi na zipi ambazo Watanzania wanaweza kutembelea moja kwa moja kwa utaratibu wa Visa on entry wakati wa kuingia ukiondoa nchi za Jumuiya ya Mashariki?

“Visa huambatana na masharti ambayo hutolewa na nchi husika ili kuwarusu raia wa kigeni kuingia au kuondoka nchini kwa muda maalum fursa hiyo inapotolewa katika vituo vya kuingilia nchini inajulikana kama Visa on arrival, utaratibu wa Visa on arrival uko katika sura ya makubaliano au Mikataba baina ya nchi na nchi au taratibu zinazotokana na matengamano na ushirikiano wa Kimataifa kikanda, utaratibu huu unaweza kubadilika kutokana na makubaliano na hali ya usalama kati ya nchi na nchi, Zipo nchi 16 ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea katika utaratibu wa Visa on arrival ya kuwa na viza na duniani zipo 67 Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea¬≠Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo pamoja na utaratibu huu wa Visa on arrival pia zipo nchi 67 duniani Watanzania wanaweza kuzitembelea bila hitaji visa,” alisema Mhe. Masauni.

“Ni kweli nchi za Jumuiya Madola zinautaratibu wa kutembeleana wananchi wake bila ya kuwa na Visaa lakini kama nilivyo jibu katika swali langu la msingi kwamba ushirikiano na matengemano hayo ya jumuiya ya madola utaratibu wake unaweza kubadilika kulingana na mahusiano na hali ya kiusalama ,kwa hiyo siyo jambo la kushangaza kuona India na Nigeria kwamba nchi hizi mbili zipo kwenye Uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini utaratibu wa visa kuna ‘level’ unakuwa hautumiki,” alisisitiza Masauni.

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments