Burudani

Serikali yatangaza kulifungia shindano la Big Brother Naija 2019, Yadaiwa linaiharibu jamii kwa vitendo vya ngono

Serikali ya Nigeria ipo kwenye mchakato wa kulifungia shindano la Big Brother Naija 2019, Hii ni baada ya matukio kadhaa yanayoonesha vitendo vya ngono wakati show hiyo ikiwa mubashara kwenye runinga.

Tayari Mamlaka ya mawasiliano nchini humo (NBC), Wameanza kuchukua hatua ikiwemo kuchunguza video zilizopelekea wananchi wengi kulalamika mitandaoni.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa na Maadili nchini Nigeria (NCAC), Otunba Segun Runsewe amedai kuwa tayari amewatumia nakala ya zuio la shindano hilo kurushwa mubashara kwenye vituo vya runinga bila kuhaririwa huku wakisubiri uchunguzi.

Mitandao nchini Nigeria kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya shindano hilo, Wengi wakitaka Serikali ifuatilie masuala muhimu kama rushwa na sio vitu vidogo kama hivyo.

Wengine pia wameenda mbali kwa kusema shindano hilo, Limetoa tahadhari kwa watazamaji ni lazime wawe na miaka 18 kwenda juu. Hivyo kwa wazazi wana jukumu la kuwalinda watoto wao.

Mvutano huo pia, Umeenda mbali zaidi hadi kwenye masuala ya kibiashara ambapo kampuni ya Startimes imetangaza kuandaa “Reality TV Show” ambayo itafuata maadili na haitaonesha uchafu kama wa Big Brother Naija.

Startimes wamechukua uamuzi huo, Ili wawanyong’onyeshe waandaaji wa shindano la Big Brother Naija ambao ni washindani wao DStv.

Mshindi wa Big Brother Naija 2019 ataibuka na kitita cha Naira milioni 60,000,000 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 380.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents