Tupo Nawe

Serikali yatangaza kumsaka Dereva aliyemgonga Twiga Mikumi, Fahamu faini utakayotozwa endapo utagonga wanyamapori hawa mbugani

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii, kuanzia jana kumekuwa na picha ya Twiga ikisambaa akiwa amegongwa na gari la mizigo, Sasa ukweli ni kwamba tukio hilo limetokea katika mbuga ya Mikumi mkoani Morogoro na tayari serikali imetangaza kumsaka dereva wa gari hilo aliyesababisha ajali.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mhifadhi Wanyamapori, Anasteria Ndaga, imesema wanamtafuta dereva huyo ambaye jina lake halijajulikana, kwa tuhuma za kumgonga na kumuua Twiga katika mbuga ya wanyama ya Mikumi.

Kwa mujibu wa sheria za wanyamapori mbugani, faini ya kumgonga mnyama Twiga akiwa Mbugani ni zaidi ya Tsh. Milioni 33.

Soma zaidi hapa chini kufahamu tahadhari na faini utakayopigwa endapo utawagonga wanyamapori, hususani kwenye barabara zilizokatiza mbugani kama ile ya Dar- Mbeya.

1. Hutakiwi kulisha wanyama au kutupa kitu kama chupa au kopo mbugani, maana unaweza leta shida kwa mnyama ataekula .

2. Hutakiwi kusababisha ajali ya aina yoyote Mbugani. Kwa kawaida spidi ya mchana mbugani ni 70km/h na usiku ni 50km/h.

Hizi ni baadhi ya faini ambazo utatozwa endapo utagonga mnyamapori mbugani na hii ni kwa hapa kwetu Tanzania.

TEMBO = USD 15,000 ~ Tsh mil 35.1
NYATI = USD 1,900~ Tsh mil 4.3
SIMBA = USD 4,900~ Tsh mil 11.3
CHUI = USD 3,500~ Tsh mil 8
TWIGA = USD 15,000~ Tsh mil 34.6
FISI = USD 550~ Tsh mil 1.2
NGIRI = USD 450~ Tsh mil 1
NYANI = USD 110~ Tsh laki 254
PUNDAMILIA = USD 1200~ Tsh mil 2.7
SWALA = USD 390~ Tsh laki 9

Na endapo ukipata ajali ndani ya Mbuga faini yake hutozwa Tsh 200,000 na ukizisha mwendo kwenye hifadhi faini yake ni Tsh . 30,000/= .

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW