Habari

Serikali yatoa majibu kuhusu sehemu zisizo na minara ya mawasiliano

Serikali inakusudia kuanisha maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara na kutangaza tenda kuweka minara ya simu ili wananchi waweze kupata mawasiliano.

Hayo yamebainishwa leo, Mei 15 Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ambapo amesema kuwa makampuni ya simu yanafanya biashara na ili waweke minara ni lazima eneo liwe na mvuto wa kibiashara.

“Mfuko wa mawasiliano wa wote ni Taasisi ya serikali ambayo inahusika kupeleka mawasiliano katika vijiji vyote ambavyo ambazo hazina mvuto wa kibiashara haya Makampuni ya simu yanafanya biashara ili yaweze kufanya biashara sehemu moja wapo ni lazima pawe na mvuto wa kibiashara, kuepuka serikali ilianzisha mfuko wa mawasiliano kwa wote kuhakikisha hata zile sehemu zisizo za kibiashara zinapata mawasiliano,” Mh. Nditie.

Aidha Ntitiye alisema atafanya ziara nchi nzima katika maeneo ambayo hayana mawasiliano haswa kwa wabunge walioleta barua ambao maeneo yao hayana mawasiliano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents